you touch africa

 

you touch africa

Gusa Afrika - Badili maisha

Miradi

 

Yaliyomo

 

Kuhusu Sisi

 

Miradi

 

Historia

 

Michango

 

Uchangiaji

 

Mawasiliano

 


Miradi

 

Miradi yetu ya mwanzo iko Tanzania, Afrika ya Mashariki, ambako tuna uelewa mkubwa na mawasiliano mazuri

 

1. Kubadilisha paa bovu la Shule ya Msingi Makomu

Shule ya Makomu na paa lenye kutu

Paa lililopo katika Shule ya Msingi ya Makomu/Kyala limeoza kwa kutu na linalika kila mahali. Litakarabatiwa kwa awamu ili kuhakikisha kuwa watoto hawavujiwi madarasani.

 

2. Kuwapatia chakula bora wanafunzi wa Shule ya Msingi Makomu, Tanzania

Chakula cha mchana shuleni

Kwa sasa wanafunzi wanakula ugali au makande, kwa kadri ya mchango wao wa mahindi. Yanapokwisha wanabaki bila chakula. Tunampango wakuongeza ubora wa chakula chao kwa kununua mboga za majani, mafuta ya kupikia and matunda kutoka kwa wenyeji.

Tumekidhiwa kwamba mradi huu utanafadhiliwa na Mr Wilbert Derk Amsterdam: Email:

3. Kuhamasisha na kutoa ushauri kwa waalimu na manesi wanaotaka kujitolea kufanya kazi Afrika

Mwalimu wakujitolea, Shule ya Msingi Makomu

Pale ambapo waalimu kutoka UK wamependa kwenda kufundisha huko Africa wakati wa likizo zao, tumeweza kuwapatia mawasiliano na ushauri muhimu. Lengo letu nikuwapa mwamsho wa kushirikiana kielimu, kati ya waalimu na watoto wa mashule ya Afirika na ya Ulaya..

 

4. Kusafirisha vifaa vya afya kwenda Afrika

Tumepewa msaada wa vifaa vya hosipitali na daktari wa Ulaya. Kwa sasa tunatafiti uwezekano wa kusafirisha vifaa hivyo kwenda Afrika, ili vipewe hosipitali zinazohitaji vifaa hivyo..

 

5. Kushirikiana na vikundi vya wanawake katika miradi yao

Tumekuwa tukishirikiana na kikundi cha Wamama Wakatoliki Tanzania (WAWATA), katika mradi wa kukopa na kulipa. Faida inayopatikana inakwenda kusaidia kulipa madeni ya wagonjwa masikini, Hosipitali ya Makomu. Tunatafiti namna ya kuupanua mradi huu.

 

6. Kuweka madirisha katika Shule za Msingi Kitowo na Napaku

Shule hizi ziko, zaidi ya kima cha 1900m juu ya usawa wa bahari.

Ni eneo labaridi sana la Tanzania. Kwa sasa shule hazina madirisha. Tunategemea kuwawekea madirisha.

 

7. Kukarabati vibao vya kuandikia katika shule za Kitowo/Napaku

Ufundishaji kwenye ubao mweusi katika shule ya Kiafrika

Vibao kadhaa vimechakaa sana. Tutakarabati na kuweka vibao vyipya.

 

 
           
 

Juu