you touch africa

 

you touch africa

Gusa Afrika - Badili maisha

Kutuhusu Sisi

 

Yaliyomo

 

Kuhusu Sisi

 

Miradi

 

Historia

 

Michango

 

Uchangiaji

 

Mawasiliano

 


Kutuhusu Sisi

 

Chimbuko la You Touch Afirca ni kikundi cha marafiki wenye upendo mkubwa na nia ya kuleta mabadiliko ya kina katika maisha ya Waafrika masikini. Wakishirikiana kwa karibu na mmisionari mzaliwa wa Africa, wametembelea na kuishi na wanavijiji majumbani kwao. Wameguswa na msimamo wa Waafrika katika kupambana na umasikini. Wanayo hamasa ya kukushirikisha wewe katika mahusiano ya karibu waliyojenga na wananchi hao.

Mtazamo Wetu

Ni mtazamo wa You Touch Africa kusimama kidete na masikini wa Africa katika kusaidia juhudi zao kwa kutumia 100% ya fedha za wafadhili katika miradi teule. Wafadhili na washiriki wa kujitolea katika You Touch Africa watakuwa na nafasi yakupewa taarifa za moja kwa moja juu ya misaada inayotolewa.

 

Malengo

Mlima Kilimanjaro

You Touch Africa imeundwa rasmi mwaka 2007. Ni chama cha fadhila cha kujitolea ambacho kitaandikishwa rasmi siku za karibuni na.

Tume ya Kuandikisha Vyama vyakujitolea. Lengo letu nikuungana na wananchi wa Afrika katika kufanikisha yafuatayo:

  1. Kupunguza magonjwa, afya mbaya na kusaidia waliouzeeni kati ya masikini waishio Afrika.
  2. Kuendeleze elimu ya watoto na watu wazima masikini waishio Afrika.
  3. Kuwapa nguvu za kifedha wale wasiojiweza, kwa kuwapatia mikopo, vifaa au huduma mbali mbali.

Tunaamini tunaweza kuwa na mafanikio ya uhakika kama kikundi cha fadhila, kwa kujipangia malengo ya uhakika, kushirikiana kwa karibu na wenyeji, na kwa kuwa waangalifu sana katika matumizi ya fedha.

 Kukamilisha Malengo

Miradi

You Touch Africa inayo ufahamu mkubwa na mahusiano ya karibu kati ya wanyeji wa Afrika na maisha yao. Hii inamaanisha kwamba tunaweza kutathmini mahitaji muhimu na vipaji vya wananchi. Kubaini wenyeji wenye uwezo na uaminifu wa kuisimamia miradi, na kuchagua miradi kwa uangalifu, ni kiini cha mafanikio yetu.

Kila inapowezekana, mali ghafi ya miradi itanunuliwa kutoka eneo husika, na ajira zote lazima ziende kwa wenyeji.

Kwa taarifa zaidi kuhusu miradi ya UTA, tafadhali bonyeza ukurasa wa "Miradi".

Usimamizi wa Fedha

You Touch Africa haina waajiriwa wa kulipwa na ofisi yenye kugharimu. Kazi zake zote zinaendeshwa na watu wakujitolea. Hatua hizi zinatuwezesha kuwa na matumizi kidogo sana. Gharama za kiuongozi na offisi zinalipwa na wanakamati na wahusishwa wengine. Hii inatuwezesha kuahidi kwamba 100% ya hela za mradi teule hazitumiki pengine.

Kwa uzoefu wetu tunajua kwamba kusimamia fedha Afrika ni muhimu sana. Kwa hilo tuko makini kushirikisha watu waaminifu, kwa nia ya uwazi na kuwajibika.

Chanzo cha Chama

Maelezo kuhusu historia ya UTA na kazi zilizofanywa na wanakamati, tafadhali bonyeza hapa.

 

Ni imani yetu kwa, kushirikiana na Waafrika katika kuinua hali ya walio masikini, ni kwa faida yetu pia.

 

   
           
 

Juu